By: Richard Mwambe
Ilipoishia
Yule mwingine aliyekuwa pale chini
kumbe alishazinduka kitambo. Akaichomoa bastola kumwelekea Amata asijue ni mtu
wa namna gani wanayepambana naye. Amata kwa haraka alimchota ngwala
yulealiyekuwa akipambana naye na wakati akianguka, ile risasi ilifumua kichwa
chake na Amata kwa kasi na ustadi alikirusha kisu kilichodidimia kwenye koo la
yule mshenzi mwingine. Amata akaangukachinikwa kishindo huku akishuhudia wawili
walewakiachana na uhai kwa maumivu makali.
“We ni Amata?” sauti ikasikika
kwenye kile kifaa cha mawasiliano.
“Zamu yako inakuja, hutonikimbia...” Amata akajibu na kutoa kile kifaa sikioni akakitupa kando. Kwa haraka akaondoka kwenye ile nyumba kwa kupitia upande wa nyuma. Akakwea ukuta na kuruka nje. Katika pachipachi za nyumba ile na nyingine. Kablahajatokeza barabarani akachungulia kwanza kwenye lile jengo la Umoja ambalo yule jahili alimwambia kuwa Binusi yupo pale. Macho yake yalishuhudia Peugeot 106 ikigeuzwa kibabe na kuondoka kwa kasi. Yeye! Akawaza.
Endeleeeaaa
By: Richard R. Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Richard R. Mwambe
By: Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania