By: Richard Mwambe
Ilipoishia.....
“Tuliambiwa
tumuue Selina, huyu tuliambiwa ni mwanamke hatari sana hapa Tanzania…”
akaeleza. Amata akashtuka kusikia hivyo. Selina ni Madam S. “Pia tulitakiwa
kumuua Kamanda Amata!” akaendelea kusema. Amata alihisi kuingiwa na ubaridi
kuanzia utosini mpaka unyayoni.
“Enhe!”
akamtaka kuendelea.
“Pia tulitakiwa
kumuua Geophrey Kisinini na Tabia Ismail,” yule bwana akaeleza pasi na
kumumunya maneno. Kamanda Amata akajikuta anaishiwa nguvu. Akameza mate na
kuitazama saa yake. Ilikuwa ikiyoyoma kuelekea saa tisa usiku. “Maiko mlikutana
naye wapi hapa Dar es salaam?” akauliza.
“Tulikutana naye
nyumbani kwake Kibada…” akajibu.
“Kibada? Ok!
Nikikwambia unipeleke unaweza?” Amata akauliza. Yule bwana akajibu kwa kutikisa
kichwa kwamba ‘ndiyo’. Wakati akihojiana na bwana huyo, tayari daktari alikuwa
amewasili na kazi ya kushona masikio ya Braison ilianza. Amata akatoka kwenye
kile chumba na kurudi katika ofisi ile ya upelelezi Mkoa. Pale akamkuta
Inspekta Simbeye peke yake.
“We mshenzi
siyo binadamu hata kidogo…” Simbeye akasema.
“Tukiwa kazini
hatuna mzaha hata kidogo. Asante mzee mi nimemaliza, sasa huyo ni wa kwenu siyo
wangu tena. Mimi niachieni yule mwingine bado sijamalizana naye,” Amata
akamwambia, “tuonane kesho, nitalutafuta,” akamwambia huku akipotelea nje.
Kamanda Amata akamchukua askari wa mapokezi na kumkabidhi vifaa vyote vya
Braison Sambala kisha yeye akaingia garini. Gina alikuwa amelala fofofo nyuma
ya usukani.
“We msichana,
amka twende…” akamwambia Gina huku akimtikisa. Gina akakurupuka na kujiweka
vizuri. Akajifikicha macho.
“Uuuuh
nimechoka sana… tunaelekea wapi, saa tisa sasa…” Gina akauliza.
“Twende
nyumbani kwako sasa tukalale…” Amata akamjibu. Gina akatabasamu na kuwasha
gari.
“Hayo ndiyo
maneno dear… nimemiss sana joto lako…”
“Endesha gari!”
✠ ✠ ✠
Nyumbani kwa
Gina, Msasani nyuma ya Supermarket ya Mayfair Plaza waliwasili saa tisa usiku.
Wakati Gina akioga na kujiandaa kupanda kitandani, mwili ukiwa chem-chem, Amata
alikuwa mezani katika chumba cha kujisomea. Juu ya meza hiyo palikuwa na simu
na kitabu kidogo cha kumbukumbu. Vilikuwa vitu alivyovitoa kwenye chumba cha
Braison Sambala. Akiwa ametingwa na simu yake, alihisi kuguswa bega.
“Mpenzi muda wa kulala sasa, twende
tafadhali,” sauti ya Gina iliyapenya masikio yake huku mkono wake mmoja ukiwa
umepita nyuma ya shingo ya Amata na vidole vya mkono huo vikipapasa kifua cha
mwanaume huyo. Amata alitaka kujibu, lakini alijikuta pumzi inamkatika.
Mwanamke huyu alizijua batano zote za Amata; wapi ya kushusha na kupandisha
sauti, wapi ya kupandisha na kushusha mapigo ya moyo na kadhalika. Hakuongea
kitu, akainuka na kuambatana na mwanamke huyo mpaka chumbani. Haikuwachukua
hata dakika kumi, wawili hao waligalagazana kitandani huku ndimi zao
zikipishana kwa ufundi mkubwa kutoka kinywa cha huyu kwenda kinywa cha
mwingine. Dakika arobaini na tano zilizofuata, kiu kilikuwa kimekatika. Gina
alijitupa aliuchapa uzingizi mzito kifuani pa Amata. Lakini mwanaume huyo bado
akili yake haikuwa sawa. Alikuwa akiwaza mengi kiasi kichwani mwake. Alitaka
kujua jambo kabla jimbi hajawaika ili ajue akitoka humo ndani ni wapi pa
kuanzia. Kokwa! Kokwa ilishaanza kumchanganya. Kichwani mwake tayari alianza
kumhitaji Chiba. Kuna mambo huyu jamaa
inabidi kuja kuyatatua! Akawaza. Akiwa katika mawazo hayo akajikuta
akibebwa na usingizi mzito hasioutegemea.
Sauti ya jimbi wa alfajiri ndiyo ilimgutusha kutoka katika usingizi huo. Alipojipapasa kifuani, hapakuwa na Gina, alipogeuza macho kuangalia pembeni, hakumuona mwanamke huyo. Amata akakurupuka na kuketi kitandani. Taa ya chumbani ilikuwa ikiwaka, mlango ulirudishiwa kama kawaida. Ni Gina tu hakuwamo mle chumbani. Akainuka na kusimama wima sakafuni. Akavuta hatua kuuelekea mlango wa kile chumba na kuufungua taratibu.
By: Richard R. Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
By: Richard Mwambe