By: Richard R. Mwambe
KOKWA...
...
Kagera
Bar Lounge, ndipo lile gari lilipokuwa limeegeshwa. Gina akatafuta mahala
pazuri ambapo isingemsumbua kutoka kama ingehitajika kufanya hivyo kwa haraka.
Wakabaki ndani kwanza.
“Tunafanyaje?
Tunamvamia ndani au tunasubiri hapa mpaka atoke?” Gina akauliza.
“Gina,
mbona una maswali sana leo vipi?” Amata akauliza.
“Nna
hamu ya kazi…”
“Sawa,
nenda ndani ya hiyo bar hakikisha unamnasa, nakupa nusu saa tu…” Amata
akamwambia.
“Sasa
nitamjuaje?” Gina akahoji kwa utulivu.
“Nenda,
mwambia DJ atangaze kuwa mwenye gari aina ya Mazda Jeusi mtajie na namba
anahitajika nje, atatoka utamuona!” Amata akatoa maelekezo.
“Kazi
ndogo sana!” Gina akajibu na kutoka kwenye lile gari huku akimwacha Amata.
Hatua zake za kike zilimfikisha kwenye mlango wa kuingia kwenye klabu ile.
Kamanda Amata alikuwa akimtazama mwanamke huyo katika kila hatua. Dakika tano
zilipita, Amata hakuona chochote kinachoendelea. Dakika kama ya nane hivi,
Amata akamwona Gina akitoka nje na kusimama kando ya lile gari. Halafu muda
mdogo baadae kijana mmoja alitoka kwenye ule ukumbi na kuliendea lile gari.
Mazungumzo ya dakika kama tatu hivi yalifuata katika ya Gina na yule kijana
kisha woye wawili wakaingia ndani. Simu ya Amata ilitetemeka. Arafa moja
iliingia. Akainyakua na kuparaza kioo chake. Kulikuwa na ujumbe kutoka kwa
Gina. Akaufungua.
‘Amekolea, natoka naye si muda’
By: richard MWAMBE
By: Richard R. Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania