KIJASHO CHEMBAMBA Sehemu ya 3

By: Richard Mwambe

0
Available Stock:

Sehemu ya tatu inaanzai hapa....

Ndani ya ofisi muhimu ambayo mheshimiwa Rais hufanya mikutano ya siri na watu wake muhimu, alikuwa akizunguka huku na huko. Moja haikai wala mbili haikai. Alitoka kona hii akaelekea ile kule. Tangu aingie hapo tayari pakiti moja la sigara aina ya Sportsman lilikwishateketea. Hodi iliyobishwa kwa utulivu ilimrudishia uhai ambao uliondoka kwa sekunde kadhaa zilizopita. Msaidizi wake akafungua mlango na mwanamke mtu mzima akaingia ndani ya ofisi ile. Mheshimiwa Rais akaitazama saa yake ya mkononi na kutikisa kichwa juu chini.

            “Keti!” alimwambia mgemi wake huku naye akikiendea kiti chake na kuketi pia. “Selina! Nashukuru umekuja kwa wakati,” akamwambia na wakati huo yule mhudumu alikuwa nje ya chumba hicho.

            “Naam nimeitikia wito,” Madam S akajibu.

            “Tumeibiwa kitu muhimu sana… na cha siri mno!” akaongea huku akifikicha macho yake. “Kokwa! Kokwa hakikuwa kitu cha kimaonesho lakini ilionekana kuwa ndiyo njia pekee ya kukihifadhi,” akasema.

            “Nakuelewa mkuu, lakini naona kama habari yenyewe unaianzia katikati…” Madam S akamwambia.

            “Doh shit! Akili yangu yote nilifikiri naongea na ADC. Ni hivi, kuna wizi umetokea usiku wa kuamkia leo pale jengo la makumbusho…”

            “Ndiyo!”

            “Kimeibwa kitu muhimu sana katika nchi yetu ambacho kwacho serikali inaweza kuendesha mitambo yote ya nyuklia iliyosimikwa katika machimbo yetu huko Bahi na Namtumbo…” akaeleza.

            “Ndiyo mkuu…” Madam S akazidi kusikiliza.

            “Unajua kuwa baada ya ugunduzi wa madini haya hadimu nchini kwetu, tuliingia mkataba na Rusia na China ili kufanya uchimbai wa awali. Na tulipojiridhisha basi tuliwapa kibali cha kuyachimba kwa mkataba maalum ambao sina haja ya kuuzungumzia. Najua unaujua vyema kabisa…” Rais akazunguma.

            “Ndiyo najua hayo yote,” Madam akaitikia...


je nini kiliendelea... fungua na jipakulie PDF yako uburudike...

View or Download Book
📘 View PDF ⬇ Download

Related Products

Product Image
MKATABA WA KIFO (Jiue Mwenyewe)

By: richard MWAMBE

Product Image
KIJASHO CHEMBAMBA - EP 01

By: Richard Mwambe

Product Image
KIJASHO CHEMBAMBA - 02

By: Richard Mwambe

Product Image
KITANZI CHA MWISHO

By: Richard Mwambe