By: Richard MWAMBE
Ilipoishia…
“Sasa kazi inaanza!” akajisemea na kuchukua
bastola kutoka kwenye lile gari, akaikagua na kuhakikisha ipo sawa. Akafyatua
kitasa cha mlango, akateremka na kulirudia lango. Sasa kamanda Amata alikuwa
akiongozwa na hasira zaidi kuliko utashi. Akatoka nje ya uzio na kuvuta hatua
kuelekea Ofisi ndogo za Bunge. Lengo lilikuwa ni kumtaka mmiliki wa hilo gari
na nani alikuwa akiendesha. Aliamini kuwa hao wangeweza kumfanya ampate Braison
Sambala. Na kupitia wao angeweza kuanza kuingia ndani ya hujuma na kugundua
tatizo. Je wanahusika na upotevu wa Kokwa
au kuna jingine? Akajiuliza.
✠ ✠ ✠
Endelea…
Mchana wa siku hiyo, wafanyakazi wachache sana walikuwa
katika ofisi zao. Wengi walikuwa wametoka kwa Chakula cha Mchana na wengine
walienda msikitini. Amata alipanda ngazi kufika ghorofa ya kwanza ambapo
alipokelewa na mwanadada mrembo aliyekuwa nyuma ya dawati la mapokezi.
“Karibu
sana kaka nikusaidie,” akamwambia Amata.
“Asante
kwa wema wako… unaonekana u mwema sana… samahani naweza kumpata mmiliki wa gari
hilo hapo chini?” akauliza.
“Lipi?”
yule mwanamke akauliza.
“Hilo
Mazda!”
“Enhe
walitakia nini mi’ ndiye mmiliki…” yule mwanadada akaeleza bila kujua lengo la
muulizaji. Kwa upande wa Amata.
“Nashukuru
kukufahamu, nahitaji tuongee biashara, mimi mgonjwa sana wa aina hii ya
magari…” Amata akasema, “Lakini sijakujua hata unaitwa nani… mimi naitwa
Jaffar,” akasema.
“Naitwa
Nuru Sembaga!”
“Nuru… unasemaje?” Amata akauliza. Nuru alipogongana macho na mwanaume huyo aliinama chini.
By: Richard Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Richard R. Mwambe