By: richard MWAMBE
MKATABA WA KIFO (Jiue Mwenyewe)
UTANGULIZI
Saa moja usiku huo, vijana wa TSA wakiwa full package walikuwa hewani na chopa la kijeshi ambalo daima hulitumia kwa kazi zao, wakielekea huko. Scoba kama kawaida yake, alikuwa akiliongoza chuma hilo. Walihakikisha wanapita upande ambao watu wanaowataka wasishtuke. Daima Chiba alikuwa akiwaangalia kupitia kompyuta yake katika mfumo wa satellite.
“Tafuta sehemu ya kutua, tumeshawaacha
nyuma!” Chiba akamwambia Scoba. Hesabu zao hazikuwa haba. Tayari walikuwa juu
ya Mto Ruaha. Scoba akatafuta eneo zuri ambalo kwalo angeweza kushusha ile
chopa. Akalipata. Katika uwanja mdogo wa kijiji cha Igagala, wakatua. Dakika
tatu zilizofuata tayari walikuwa nje wakiwasubiri, bunduki nzito zilikuwa
vifuani mwa Kamanda Amata na Chiba na Gina huku wakiwa wamevalia mavazi ya kijeshi.
Siku mojamoja walipenda kuvaa namna hii.
Kutoka kwenye moja ya kona zilizo pembezoni mwa milima hiyo ya Tao la Mashariki, mwanga wa taa za magari yaliyokuwa yakija ili kupita eneo hilo ulionekana. Baada ya kupita lori la mafuta na mizigo. Amata na Chiba waliingia barabarani na kusimama katikati. Naam, Landrover Count, mbili, nyeusi ziliibuka.
“Haohao!” Chiba akawaambia wenzake. Wakaziweka bunduki zao tayari. Scoba akasogea na kuwasimamisha. Yale magari yakatii amri na kusimama. Scoba akaliendea lile la mbele na kugonga kioo huku akitoa ishara ya kufunguliwa kioo hicho. Kikashushwa.
“Washa taa za ndani!” akawaamuru. Yule
dereva akatii. Ndani ya lile gari mulikuwa na watu watatu, Wazungu; wawili
wanaume na mmoja mwanamke. Scoba akawaangalia vizuri. Akawahoji maswali kadhaa
kasha akawataka kushuka kufungua sehemu ya nyuma ya magari hayo.
“Mnataka nini?” Mzungu aliyekuwa
akiendesha akauliza.
“Ukaguzi! Tunataka kukagua magari yenu! Shuka haraka!” Scoba akamwambia na yule jamaa akashuka akifuatiwa na wenzake. Katika gari la nyuma, kulikuwa na wengine wawili. Magari yale yote mawili upande wa nyuma yalifungwa barabara. Mtu wa nje hasingeweza kuona vilivyomo ndani.
“Sawa!” yule jamaa akajibu na kuzunguka
nyuma ya lile gari huku Scoba akimfuata nyuma na bunduki yake ikiwa tayari kwa
lolote. Amata na Chiba nao walifuata upande huu na ule. Katika gari la pili,
hakuna aliyeshuka, lakini tayari waliona hali ya pale haina amani.
“Fungua!” Scoba akamwamuru yule jamaa
naye akafungua ule mlango. “Weka mikono juu! Mtie pingu!” Scoba akamwambia
Chiba. Scoba aliamuru baada ya kuona shehena ya bunduki hatari zilizopangwa
kwenye rafu za chuma. Yule jamaa akatiwa pingu, na waliobaki nao wakashushwa na
kutiwa pingu. Kutoka gari la pili wakajiandaa kwa mashambulizi. Mmoja wa wale
waliokuwamo humo akaandaa bastola, tayari. Akampatia mwenzake na kumweka
tayari. Wakati Scoba, Chiba na Amata wakishughulika na wale watu waliowakamata
hawa jamaa wawili waliobaki kwenye gari jingine walitoka ghafla ili kuanzisha
mashambulizi. Aliyekuwa nyuma ya usukani alipokanyaga ardhi tu, hata kabla
hajakanyaga vizuri ardhi, yule jamaa alijikuta akitupwa upande mwingine na
kuanguka kama mzigo. Roho yake ikauacha mwili. Risasi iliyopigwa kutoka
mafichoni kwenya vichaka ilimaliza kazi iliyotumwa. Yule mtu wa pili alipoona
mwenzake damu zikimruka akajua tayari, kumekucha, alicofanikiwa ni kufyatua
risasi moja ambayo badala ya kumpata mlengwa ambaye ni Scoba, ikadidimia
shingoni mwa mwenzake aliyekuwa na pingu mikononi. Kiwewe!
“Nooooo!” akapiga kelele na kujitoa
kwenye ule mlango huku akifyatua risasi ovyo. Kabla hajaleta madhara, alijikuta
akipaishwa juu na kubwagwa ukingoni mwa gema kubwa linaloelekea mto Ruaha. Gina
alijitokeza lutoka kwenye moja ya kichaka akipiga mluzi.
“Hongera mwanamke!” Amata akamwampongeza.
“Asante!”
Nusu saa baadae gari la polisi likawasili mahali pale. Askari kutoka Mikumi, wakawasili wakiwa wametimia kwa zana. Wakatakiwa kufanya wanaloweza yale magari mawili yafikishwe kituoni kabla hayajarudishwa Dar es salaam. Zile maiti mbili na wale wengine wakapakiwa kwenye lile chopa na safari ya Dar es salaam ikaanza.
Endelea kusoma riwaya hii bure kabisa...
By: Richard Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Richard R. Mwambe
By: Richard Mwambe