K.O.K.W.A Sehemu ya 07

By: Richard R. Mwambe

0
Available Stock:

KOKWA...

... 


Kagera Bar Lounge, ndipo lile gari lilipokuwa limeegeshwa. Gina akatafuta mahala pazuri ambapo isingemsumbua kutoka kama ingehitajika kufanya hivyo kwa haraka. Wakabaki ndani kwanza.

“Tunafanyaje? Tunamvamia ndani au tunasubiri hapa mpaka atoke?” Gina akauliza.

“Gina, mbona una maswali sana leo vipi?” Amata akauliza.

“Nna hamu ya kazi…”

“Sawa, nenda ndani ya hiyo bar hakikisha unamnasa, nakupa nusu saa tu…” Amata akamwambia.

“Sasa nitamjuaje?” Gina akahoji kwa utulivu.

“Nenda, mwambia DJ atangaze kuwa mwenye gari aina ya Mazda Jeusi mtajie na namba anahitajika nje, atatoka utamuona!” Amata akatoa maelekezo.

“Kazi ndogo sana!” Gina akajibu na kutoka kwenye lile gari huku akimwacha Amata. Hatua zake za kike zilimfikisha kwenye mlango wa kuingia kwenye klabu ile. Kamanda Amata alikuwa akimtazama mwanamke huyo katika kila hatua. Dakika tano zilipita, Amata hakuona chochote kinachoendelea. Dakika kama ya nane hivi, Amata akamwona Gina akitoka nje na kusimama kando ya lile gari. Halafu muda mdogo baadae kijana mmoja alitoka kwenye ule ukumbi na kuliendea lile gari. Mazungumzo ya dakika kama tatu hivi yalifuata katika ya Gina na yule kijana kisha woye wawili wakaingia ndani. Simu ya Amata ilitetemeka. Arafa moja iliingia. Akainyakua na kuparaza kioo chake. Kulikuwa na ujumbe kutoka kwa Gina. Akaufungua.

           

‘Amekolea, natoka naye si muda’

View or Download Book
📘 View PDF ⬇ Download

Related Products

Product Image
Dira Ya Maendeleo 2050

By: Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania

Product Image
KITANZI CHA MWISHO

By: Richard Mwambe

Product Image
PASIPOTI YA GAIDI - Kitabu Cha 1

By: Richard Mwambe

Product Image
MKATABA WA KIFO (Jiue Mwenyewe)

By: richard MWAMBE