By: Richard Mwambe
Sehemu ya tatu inaanzai hapa....
Ndani ya ofisi muhimu ambayo
mheshimiwa Rais hufanya mikutano ya siri na watu wake muhimu, alikuwa
akizunguka huku na huko. Moja haikai wala mbili haikai. Alitoka kona hii
akaelekea ile kule. Tangu aingie hapo tayari pakiti moja la sigara aina ya
Sportsman lilikwishateketea. Hodi iliyobishwa kwa utulivu ilimrudishia uhai
ambao uliondoka kwa sekunde kadhaa zilizopita. Msaidizi wake akafungua mlango
na mwanamke mtu mzima akaingia ndani ya ofisi ile. Mheshimiwa Rais akaitazama
saa yake ya mkononi na kutikisa kichwa juu chini.
“Keti!”
alimwambia mgemi wake huku naye akikiendea kiti chake na kuketi pia. “Selina!
Nashukuru umekuja kwa wakati,” akamwambia na wakati huo yule mhudumu alikuwa
nje ya chumba hicho.
“Naam
nimeitikia wito,” Madam S akajibu.
“Tumeibiwa
kitu muhimu sana… na cha siri mno!” akaongea huku akifikicha macho yake.
“Kokwa! Kokwa hakikuwa kitu cha kimaonesho lakini ilionekana kuwa ndiyo njia
pekee ya kukihifadhi,” akasema.
“Nakuelewa
mkuu, lakini naona kama habari yenyewe unaianzia katikati…” Madam S akamwambia.
“Doh
shit! Akili yangu yote nilifikiri naongea na ADC. Ni hivi, kuna wizi umetokea
usiku wa kuamkia leo pale jengo la makumbusho…”
“Ndiyo!”
“Kimeibwa
kitu muhimu sana katika nchi yetu ambacho kwacho serikali inaweza kuendesha
mitambo yote ya nyuklia iliyosimikwa katika machimbo yetu huko Bahi na
Namtumbo…” akaeleza.
“Ndiyo
mkuu…” Madam S akazidi kusikiliza.
“Unajua
kuwa baada ya ugunduzi wa madini haya hadimu nchini kwetu, tuliingia mkataba na
Rusia na China ili kufanya uchimbai wa awali. Na tulipojiridhisha basi tuliwapa
kibali cha kuyachimba kwa mkataba maalum ambao sina haja ya kuuzungumzia. Najua
unaujua vyema kabisa…” Rais akazunguma.
“Ndiyo najua hayo yote,” Madam akaitikia...
je nini kiliendelea... fungua na jipakulie PDF yako uburudike...
By: Richard Mwambe
By: Richard R. Mwambe
By: Richard Mwambe
By: Richard Mwambe